Madhumuni Ya Chama Kikuu

Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Shinyanga SHIRECU (1984 LTD kiliundwa kwa madhumuni yafuatayo kwa mujibu wa Masharti ya Chama kama ifuatavyo:-

1) Kustawisha hali ya uchumi ya wanachama wake kwa kufanya mipango ya kuendeleza shughuli za kilimo cha zao la Pambana mazao mengine, zinazoendeshwa na Vyama vilivyojiunga nacho kwa hiari na kwa kufuata misingi na taratibu za Vyama vya Ushirika.

2) Ili kutekeleza madhumuni yaliyotajwa hapo juu, Chama kitafanya mambo yafuatayo:-

a. Kuendeleza shughuli za Ushirika kwa wanachama wake na kuhamasisha Vyama vya Msingi vilivyo katika eneo la shughuli zake vijiunge na chama.

b. Kutoa Elimu ya Ushirika na kilimo bora kwa Wanachama wake, Viongozi na Watendaji wa Chama.

c. Kushirikiana na wanachama wake kukusanya, kuhifadhi, pamoja na kutafuta masoko ya Pamba na mazao mengine kwa lengo la kuwapatia bei nzuri kwa faida ya wanachama wake.

d. Kununua na au, kukodi ardhi, majengo, magari, mitambo, maghala, maofisi, na vifaa mbali mbali kwa matumizi yake na wanachama wake.

e. Kununua, kuuza na kusambaza pembejeo za kilimo kwa wanachama wake kwa bei nafuu ili kuboresha kilimo cha Pamba na mazao mengine ya kilimo.

f. Kutoa mikopo na misaada ya kifedha, kwa wanachama wake kwa kufuatana na masharti haya, Sheria ya Vyama vya Ushirika Na. 6 ya mwaka 2013 pamoja na Kanuni zake za mwaka 2015 pamoja na marekebisho na miongozo ya kisheria inayotolewa na Mrajis wa Vyama Ushirika nchini.

g. Kuwekeza katika Vyama vingine vya Ushirika vyenye dhima ya kikomo, taasisi za kibiashara kwa minajili ya kukipatia faida Chama kulingana na Sheria ya Vyama vya Ushirika Na. 6 ya mwaka 2013 na Kanuni zake za mwaka 2015.

h. Kutoa ushauri, kuelekeza na kusimamia Vyama wanachama katika kutayarisha Makisio ya Mapato na Matumizi.

i. Kufanya mambo mengine yaliyo halali na ambayo ni ya lazima katika kuendeleza kazi zilizotajwa hapo juu katika kufanikisha utekelezaji wa madhumuni ya Chama kama yatakavyopitishwa na Mkutano Mkuu na kama Sheria ya Vyama vya Ushirika Na. 6 ya mwaka 2013 na Kanuni zake za mwaka 2015 zinavyoelekeza.

j. Kuyaongezea thamani mazao ya wanachama kabla ya kuyatafutia masoko.