MRJIS AUTAKA CHAMA MKUU WA SHIRECU KUONGEZA TIJA KATIKA UENDESHAJI.

MRJIS AUTAKA CHAMA MKUU WA SHIRECU KUONGEZA TIJA KATIKA UENDESHAJI.

MRJIS AUTAKA CHAMA MKUU WA SHIRECU KUONGEZA TIJA KATIKA UENDESHAJI.

Mrajisi na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), Dk Benson Ndiege amewataka watendaji kuendelea kuweka maslahi ya wanachama mbele katika utendaji wao ili kuleta manufaa kwenye Ushirika.

Hayo ameyasema wakati akitembelea mabanda ya Wadau wa Vyama na Ushirika Julai 3, 2024 katika Viwanja vya Ipl, Tabora.

Aidha, Msajili ametoa ushauri, mapendekezo na maelekezo mbalimbali kuhusu baadhi ya changamoto za chama pamoja na kuwapongeza kwa mafanikio katika vyama.

Miongoni mwa mambo aliyoagiza yashughulikiwe ndani ya chama ni pamoja na kuhakikisha chama kinafanya kazi kwa bidii ili kuwa na Cheti Safi, kuongeza miundombinu ya kuongeza thamani ya bidhaa, kukuza bidhaa za chama na kujifunza kutoka kwa vyama vingine.

Go Back