UMUHIMU WA USHIRIKA MKOANI SHINYANGA

Ushirika ndiyo silaha pekee iliyobaki na ya kutegemewa ili kumwinua Mkulima wa hali ya chini, kupitia Ushirika Wakulima huwa na sauti moja katika kuamua mambo kama kupanga bei ya mazao yao pindi wanapotaka kuuza, kutafuta soko la uhakika, ikiwa ni pamoja na kuzalisha kwa tija. Aidha kupitia Ushirika wakulima kwa kiasi kikubwa hupata faida kubwa kwani wao ndio hupanga bei mfano mzuri ni kupitia mfumo wa Stakabadhi ghalani.

  • Kupitia Ushirika mfano kwa mkoa wa Shinyanga Mkulima atapata faida kubwa sana kwani licha ya kuwa na zao la Pamba kwa muda sasa, Serikali imerasimisha rasmi zao la Dengu na Choroko pia kuuzwa kwa njia ya Minada na hivyo kuongeza pato kwa Mkulima wa chini.

 

  • Ongezeko la uelewa na umuhimu wa Mkulima kutumia Ushirika ili kupata tija na kuepuka kuibiwa ama kupata hasara. Mfano kwa mwaka 2020/2021 SHIRECU (1984) LTD imepanga kutumia mfumo wa Stakabadhi ghalani kwa Mkulima kuuza mazao yake mfumo ambao kimsingi ni agizo la Serikali yetu pendwa ya Awamu ya tano.