LENIS JISHANGA IZENGO, Mwenyekiti wa Chama kikuu cha Ushirika [SHIRECU (1984) LTD]
NAOMI MAYEGA CHABA, Makamu Mwenyekiti wa chama kikuu cha Ushirika [SHIRECU (1984) LTD]

Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Shinyanga SHIRECU (1984) LTD kilisajiliwa tarehe 4 April, 1984 na kupewa Hati ya Usajili Namba 4123. Hata hivyo, kulingana na mabadiliko ya Mfumo wa uendeshaji wa Vyama vya Ushirika (MUVU) mnamo mwaka 2022, Chama kilifanikiwa kupata usajili mpya wenye namba AFF-SHY-SHY-MC-2022-9. Kwa sasa SHIRECU (1984) LTD inaundwa na Vyama vya Msingi 107 vinavyojishughulisha zaidi na zao la Pamba na mazao mengine mchanganyiko kwa maana ya Dengu na Choroko. Aidha, Chama kina jumla ya wanachama zaidi ya 38,178 ambao ndio wanaunda Vyama vya Msingi 107.